Bringing you news from all corners of Kenya.|Sunday, September 23, 2018
You are here: Home » All Articles » Counties » Bungoma » Mamlaka ya mawasiliano kupambana na semi za chuki kwenye mitandao

Mamlaka ya mawasiliano kupambana na semi za chuki kwenye mitandao 
Mamlaka ya Mawasiliano nchini imeweka mikakati mwafaka ya kupambana na matamshi ya chuki kwenye mitandao ya kijamii haswa wakati huu ambapo taifa linajiandaa kwa marudio ya kura za uchaguzi wa urais.

Mkurugenzi Mkuui  wa mamlaka hiyo, Francis Wangusi, amesema tume hiyo inaendeleza juhudi za kuhakikisha kuwa wananchi hawagawanywi kupitia matamshi ya uchochezi ambayo mara nyingi huenezwa kupitia mitandao ya kijamii.

Aidha amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza visa vya uchochezi kwenye mitandao ya kijamii, na kuongeza kuwa ana imani kwamba kura za marudio ya uchaguzi wa urais, zitafanyika kwa njia ya amani.

Wangusi alikuwa akizungumza kwenye hafla ya kuchangisha fedha, katika shule ya upili ya wavulana ya Namwela eneo bunge la Sirisia ambapo alisisitiza umuhimu wa elimu katika jamii, kama njia ya pekee ya kuondoa umasikini.

Vile vile alifichua kuwepo kwa mradi wa kuwezesha shule zote za upili kote nchini kuwa na mtandao akisema tayari shughuli hiyo imeanzishwa katika Kaunti ya Bungoma, ambapo shule hamsini na nne (54) za mbeleni zinatarajiwa kunufaika.

Na  Roseland  Lumwamu

Related posts:

Leave a Response