Bringing you news from all corners of Kenya.|Saturday, September 22, 2018
You are here: Home » All Articles » Editor's Picks » Sofapaka yapata matumaini ya kung’aa ligini baada ya kupata ushindi dhidi ya AFC

Sofapaka yapata matumaini ya kung’aa ligini baada ya kupata ushindi dhidi ya AFC 
Sofapaka  imefufua matumaini yake kwenye ligi ya mwaka huu kwa kupiku AFC Leopards mabao mawili kwa moja kwenye mechi iliyochezwa jana uwanjani Narok.

Hii ni baada ya Sofa Paka maarufu kama ‘batoto ba Mungu’ kukosa kuandikisha ushindi kwenye mechi ya awali na Mathare United FC ambapo walichapwa mabao tatu kwa moja Jumapili iliyopita.

Ukurasa wa matumaini ulifunguliwa na mshambulizi gwiji wa Sofapaka, Kasumba Umaru kwenye dakika ya pili licha ya kudaiwa kuugua.

Aidha, Leopards maarufu kama ‘Ingwe’ ilijaribu kuzima juhudi za Sofapaka kwenye dakika ya 25 kupitia, Ezekiel  Odero aliyefunga bao kwa bahati ya mtende.

Yamkini mkwaju wake uliokuwa ukififia ulipita na kuingia wavuni kabla ya kipa wa Sofapaka, Kigonya Mathias kuilalia kwa ustadi wake wa kawaida.

Vile vile kwenye awamu ya pili Kimani Kevin aliipa Sofapaka bao la pili katika dakika ya 60.

Mechi ilikamilika Sofapaka ikiwa mbele kwa mabao mawili kwa moja huku Kocha wa Sofapaka, Sammy  Simwa akipongeza ushindi huo na kudai atatia bidii.

Wakati huo, Robert  Matano, Mkufunzi  wa  AFC amedai kikosi chake kilichoka, kando na kukosa mpangilio mwema.

Ni mara ya pili sasa Sofapaka kushinda AFC leopards uwanjani Narok Stadium kwani katika msimu wa mwaka jana Sofapaka iliishinda AFC.

Na  Ann  Salaton

Related posts:

Leave a Response