Bringing you news from all corners of Kenya.|Thursday, August 16, 2018
You are here: Home » All Articles » Gender & Children Issues » Mwanamasumbi mstaafu aitaka kaunti ya Vihiga kuwekeza katika ndondi

Mwanamasumbi mstaafu aitaka kaunti ya Vihiga kuwekeza katika ndondi 
Serikali ya kaunti ya Vihiga imetakiwa kuweka mikakati ya kukuza vipaji vya vijana, haswa masumbwi, kama njia mbadala ya kukabiliana naukosefu wa ajira pamoja na kuongezeka kwa visa vya uhalifu.

Haya ni kwa mujibu wa Bwana Peter  Okusimba, mwanamasumbwi wa kimataifa ambaye amestaafu, alipoongea na shirika la habari la Kenya News Agency (KNA) katika mkahawa mmoja jijini Luanda siku ya Jumamosi.

Okusimba alilaumu kudorora kwa michezo nchini, haswa masumbi, kwa kile alichodai kama mipangilio duni katika idara ya michezo na utamaduni.

“Ni jambo la kuvunja moyo sana kwa nchi tajika kama Kenya kukosa kuzoa nishani za dhahabu katika michezo ya jumuia ya madola iliyokamilika hivi karibuni Gold Coast, Australia” alisema Okusimba, ambaye alimpongeza

mwanandondi Christine Ongare aliyeshinda nishani ya shaba katika michezo hiya.

“Hii ni kinyume na miaka ya tisaini wakati wanamasumbi wa Kenya walikuwa wakingaa na kuiletea inchi sifa sufufu katika michezo ya kimataifa,” aliongeza kusema Okusimba.

Usemi wa Okusimba ulioungwa mkono na Bwana Josphat Oguda, mshirikishi wa michezo ya ndondi kaunti ya Vihiga.

Oguda alilama kwamba licha ya serikali ya kaunti kutenga shilling 1.7milioni kwa kila wadi kwa ajili ya kuendeleza sekta ya spoti hakuna mipangilio maalumu ya kukuza na kuboresha mchezo wa ndondi.

Oguda ametoa mwito kwa Gavana Wilbur Ottichilo kuingilia kati ili kusaidia kurekebishwa swala hilo.

“Ndondi ni mojawapo wa michezo ambayo inayo uwezo wa kuiletea sifa kuu kaunti ya Vihiga ,” alinukuliwa Oguda.

Aidha, baadhi ya wakazi wa kaunti hiyo walioongea na KNA walitilia mkazo swala la udumishaji michezo ya aina mbali mbali, huku wengi wao wakihoji kuwa licha ya kutoa ajira kwa vijana, michezo pia huchangia

muno katika ukuzaji wa maadili mema katika jamii.

Na  Maurice  Aluda

 

Related posts:

Leave a Response