Bringing you news from all corners of Kenya.|Wednesday, September 19, 2018
You are here: Home » All Articles » Wakaazi wa Kikuyu waadhimisha sherehe za Madaraka.

Wakaazi wa Kikuyu waadhimisha sherehe za Madaraka. 
Serikali ya Kaunti Kiambu imenunua dawa za shilingi milioni 140 zitakazopelekwa katika hospitali mbalimbali zioko katika Kaunti ndogo 12 za Kaunti ya Kiambu.

Bali na hayo, serikali hii ikishirikiana na AMREF imezindua usajili wa wakaazi wa Kiambu katika bima ya afya National Hospital Insurance Fund (NHIF) itakayoweza kunufaisha wakaazi kupata matibabu.

Akisema kuwa ni sharti wakaazi waweze kujimudu kwa matibabu yaliyoboreshwa Gavana wa Kiambu Bwana Ferdinand Waititu aliwaahidi wakaazi wa Kaunti kuwa serikali yake itaendelea kutia jeki katika sekta ya afya ili iwanufaishe wote haswa wasiokuwa na mapato ya kikamilifu.

Akimwakilisha gavana Waititu katika sherehe za kuadhimisha sikukuu ya Madaraka katika uwanja wa shule ya msingi ya Kikuyu Township, ambapo mamia ya wakaazi na wanafunzi kutoka shule kadhaa kutoka maeneo bunge ya Kikuyu na Kabete walifurika wakiungana na Wananchi katika Sehemu nyingine nchini.

Hivi karibuni, gavana Waititu amewaahidi wakaazi kuwa huduma za Dialysis zitaanza kupewa wagonjwa wanaohitaji katika hospitali kuu ya Thika ambako tayari mashine zimewekwa”akisema bwana Kingori.

Isitoshe, sawa na agenda nne kuu za serikali kuu, kaunti ya Kiambu imetenga ardhi ambayo nyumba 1300 zitajengwa katika maeneo bunge ya Thika, Ruiru na Kiambu ili kutoa makao  nafuu kwa wakaazi katika mwaka wa fedha 2018-2019, gavana asema.

Wakulima wa mifugo hawakuachwa nyuma kwani gavana alisema kuwa serikali yake inatarajia kuanza ununuzi wa maziwa kutoka kwa wakulima hawa na kupatia watoto shuleni ili yaweze kuwaondolea njaa wanapokuwa wakipata masomo.

Kwa kufanya hivi, wakulima hawa watapata soko la kudumu la maziwa na pia kuwalisha watoto shuleni, gavana alifichua.

Gavana Waititu alisema kuwa vita dhidi ya pombe haramu itaendelea na leseni za uuzaji pombe zitakabidhiwa  tuu wafanyibiashara ambawo wametii sheria katika utendakazi wao.

Bwana Waititu alionya kuwa serikali yake haitaleza kamba kuwaandama wanaovunja sheria ili kujinufaisha kwa kuuza pombe haramu inayoharibu vijana wetu.Huku hutuba yake ikisomwa kwingineko, walionusuriwa kutoka katika zimwi la pombe haramu walivalia nguo rasmi iliyo na maandishi “Sasa nimekuwa soba” katika shehehe za Madaraka zilizoandiliwa katika uwanja wa Ndumberi.Gavana aliwafurahia watu hao na kuwaita ili wasongee jukwa na wengine wakipigania kumsalimu bwana Waititu.

Kingori alitamatisha Kwa kutangaza numbari ya dharura ambayo wakaazi wanaweza kupiga kufuatia tukio la dharura ambayo itafanya kazi kwa masaa 24 kwa wiki. Numbari hiyo ni 0800722382.

Baada ya hotuba ya gavana, kaimu kamishina wa kaunti ya Kiambu Bwana Paul Famba aliisoma hotuba ya raisi na hapo baadaye kauli mbiu ikawa upanzi wa miti ambapo watu waliandamana kupanda miti.

Bw. Famba aliwahimiza wakaazi kuendeleza upanzi wa miti majumbani mwao akisisitiza kuwa ulinzi wa mazingira ulikuwa jukumu letu sote kama Wananchi wanaotakia vizazi vyetu vya baadaye maisha mazuri.

Hafla zote za sherehe hii zilifika kileleni wakati waliohudhuria walipewa mlo kwa soda na mikate na baadae kutawanyika baada ya siku iliyofurahikiwa na wengi.

Lydia Shiroya Na Winnie Kimani

 

 

Related posts:

Leave a Response