Bringing you news from all corners of Kenya.|Wednesday, September 20, 2017
You are here: Home » All Articles » Counties » Vihiga » Serikali ya kitaifa yaombwa kuimarisha mradi wa NYS Vihiga

Serikali ya kitaifa yaombwa kuimarisha mradi wa NYS Vihiga 

Special Programmes Principal Secretary (PS), Josephta Mukobe
addressing youth at Elukongo market in Emuhaya sub county during
official launch of Youth Empowerment Programme for Vihiga and Emuhaya
sub counties on Friday
Youths from Vihiga and Emuhaya sub counties at Elukongo market celebrating launch of Youth Empowerment Programme on Friday

Youths from Vihiga and Emuhaya sub counties at Elukongo market
celebrating launch of Youth Empowerment Programme on Friday

Serikali ya kitaifa imetakiwa iimarisha mpango wa huduma mashinani chini ya National Youth Service (NYS) katika kaunti ya Vihiga kama njia moja ya kuwasaidia vijana wengi kupata mafunzo ya kujikwamua kutoka kwa lindi la umaskini.

Haya ni kwa mujibu wa Bwana George Atetwe anayewania kiti cha ubunge cha kaunti ndogo ya Luanda kupitia chama cha Jubilee (JP).

Atetwe alisema huduma hiyo ya vijana haijawahusisha vijana kutoka kaunti ya Vihiga kikamilifu, akiongezea vijana sehemu hiyo wamesalia kunung’unika kwa kutojumuishwa katika mradi wa kuwainuia, ilmaarufu Youth Empowerment Programme.

Ni usemi ulioungwa mkono na Bwana Caleb Ingolo ambaye anawania ubunge wa Emuhaya kwa tiketi chama chaJubilee.

Ingolo ameitaka idara husika kuongeza idadi ya vijana wanaochukuliwa kwa mradi wa NYS kutoka 500 hadi 1000 katika kila kaunti ndogo tano za Vihiga.

Kwa upande wake, katibu mkuu kwa wizara ya mipango maalum (Special Programmes) Bi Josephta Mukobe alisema takriban kaunti ndogo 117 zimefikiwa na mradi huo wa NYS.

Akisifia mradi wa NYS, Bi Mukobe alisema umewasaidia vijana kupata mafunzo maalum yatakayowasaidia kujiajiri ama kuwa katika nafasi bora kuajiriwa.

Bi Mukobe alidokeza kwamba atashauriana na waziri wa Utumishi wa Umma na Vijana, Bi Sicily Kariuki na kuhakikisha kaunti ndogo za Hamisi, Luanda na Sabatia katika kaunti ya vihiga ambayo hayajafikiwa yamefikiwa na mradi wa NYS.

Viongozi hao walikuwa wakiongea katika soko la Elukongo, kaunti ndogo ya Emuhaya wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa Youth Empowerment Programme kaunti ndogo za Vihiga na Emuhaya siku ya Ijumaa.

Bi Mukobe alimwakilisha Waziri Sicily Kariuki.

Na Maurice Aluda

Related posts:

Leave a Response